×

Mwanza: Mahabusu 2, Mfungwa Wauawa Wakitoroka – Video

MAHABUSU wawili  na mfungwa mmoja wamefariki dunia wakati wakijaribu kutoroka katika gereza kuu la Butimba jijini Mwanza walipokuwa wakishikiliwa kwa makosa tofauti ikiwemo mauaji na uhujumu uchumi.

Taarifa ya Jeshi la Polisi mkoani Mwanza imesema Aprili,  14, 2020, majira ya saa 12:30 asubuhi watuhumiwa Yusuph Bernard na Seleman Seif walijaribu kutoroka kwenye gereza hilo.

Askari magereza wakishirikiana na wananchi waliwakimbiza na kufanikiwa kuwakamata ambapo wananchi waliwashambulia kwa kipigo katika sehemu za miili yao na kusababisha  hali zao kuwa mbaya ambapo  walipelekwa hospitali ya Mkoa wa Mwanza, Sekou Toure kwa ajili ya matibabu, lakini majira ya walifariki dunia jioni  wakati wakiendelea na matibabu.

Mtuhumiwa wa tatu katika utoro huo, George  aliyekuwa amefungwa kwa kosa la uhujumu uchumi  na kifungo kingine cha kutoroka chini ya ulinzi, baada ya kukamatwa katika jaribio hilo la kutoroka tena alianza kukimbia ndipo askari  walimrushia risasi miguuni na kufanikiwa kumkamata na alifariki pia Hospitali ya Seko Toure  alikopelekwa kwa matibabu.

Leave a Comment