×

Meneja Ataja Timu Anayokwenda Ajibu

MENEJAwa nyota wa klabu ya soka ya Simba Ibrahim Ajibu, Hanii Kessy, amesema kuwa kwa sasa mipango yao ni kumtafutia mteja wake nafasi ya kucheza soka la kulipwa nje ya mipaka ya Tanzania.

 

Ajibu amekuwa hapati nafasi ya kutosha ndani ya Simba msimu huu tangu alipojiunga nayo akitokea Yanga kutokana na ushindani mkubwa wa namba ndani ya kikosi hicho.

 

Akizungumzia kuhusu majaaliwa ya Ajibu ndani ya kikosi cha Simba, Kessy alisema: “Kwa sasa malengo yetu ni kumtafutia Ajibu nafasi ya kwenda kucheza soka la kulipwa nje ya Tanzania.

 

“Tayari tumeshapokea ofa za klabu tofauti kutoka nje ya Tanzania lakini kwa kuwa mteja wetu bado ana mkataba na Simba hivyo tumewaomba wafuate utaratibu wa kuongea na klabu kwanza,” alisema bosi huyo.

 

Takwimu za Ajibu msimu huu zinaonyesha mpaka sasa kwenye Ligi Kuu Bara ameifungia Simba bao moja na kutoa pasi nne za mabao.

Stori na Joel Thomas, Championi

Leave a Comment