
SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba ameweza kukiongoza kikosi chake kuweka rekodi za kibabe ndani ya Ligi Kuu Bara kwa kuwakimbiza wapinzani wake wote 19 ndani ya ligi.
Ikiwa imetwaa ubingwa mapema ikiwa imebakiza mechi sita mkononi kwa sasa ina mechi mbili baada ya kucheza mechi 36 ina pointi 84 kibindoni inaweza kumaliza ikiwa na pointi 90 kama itashinda mechi zake mbili zilizobaki, kesho itamenyana na Coastal Union Uwanja wa Mkwakwani Tanga na itamalizana na Polisi Tanzania zote ugenini.

Kwa upande wa mabao ya kufunga, Simba inakimbiza ikiwa na mabao 76 ya kufunga huku ikiwa imefungwa mabao 20 ambayo ni machache ndani ya dakika 3,240 ilizotumia uwanjani ikiwa na wastani wa kufunga bao moja kila baada ya dakika 72, na ikiokota nyavuni bao kila baada ya dakika 162.
Mbali na kuwa vinara kwa kutupia mabao pia kinara wa utupiaji ndani ya ligi ni Meddie Kagere mwenye mabao 22 anafuatiwa kwa ukaribu na mzawa Yusuph Mhilu anayekipiga Kagera Sugar ana mabao 13.

Mtengeneza mipango namba moja ndani ya ligi ni Clatous Chama mwenye pasi 9 na ana mabao mawili kibindoni, anafuatiwa na Francis Kahata wa Simba.
Yanga imewashika shati Simba kwenye upande wa mechi za kupoteza ambapo wote wamepoteza jumla ya mechi nne. Simba imenyooshwa na Mwadui FC, JKT Tanzania, Yanga na Mbao