
Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA), Eng. Deusdedit Kakoko, kuna watumishi wachache wa bandari bado hawajabadilika ambapo wapo baadhi yao wamesimamishwa kazi na wengine mashauri yao yanaendelea kusikilizwa.
Eng. Kakoko amempongeza Mbunge wa Buchosa, Mhe. Eric Shigongo kwa kufatilia na kubaini changamoto za bei kubwa zinazotozwa na TPA kwa wananchi wanaotumia Bandari ya Kanyara.
Aidha, Eng. Kakoko amesema tayari TPA imeshafanya uchunguzi na kubaini gharama hizo ni kubwa hivyo amemwahidi mbunge huyo pamoja na wananchi wa maeneo ya bandari za Ziwa Victoria na maziwa mengine nchini kuwa bei hizo zitapunguzwa. “Tunasubiri vikao vipitishe, ninamhakikishia Mhe. Shigongo, bei hizo zitapunguzwa…”