×

Live: Global Habari Febr 11 – JPM Atoa Maagizo Soko La Morogoro..

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Magufuli ametoa maagizo kwa Wizara ya TAMISEMI pamoja na Viongozi wa Mkoa wa Morogoro kuhakikisha wanasimamia watumishi wa manispaa waliochukua fedha za vizimba kwa wafanyabiashara kinyume cha utaratibu uliowekwa.

Rais Dkt John Pombe Magufuli ametoa kauli hiyo hii leo wakati akizindua Soko la kisasa mkoani Mororgoro ambapo ameonesha kusikitishwa na baadhi ya watumishi wa Manispaa kuchukua fedha za vizimba kinyume cha utaratibu uliowekwa Aidha Dk.Magufuli amebadilisha jina la soko kuu la Morogoro na kuliita soko la chifu Kingalu ambaye alikuwa chifu wa waluguru huku akiwataka watanzania kulima sambamba na kuchukua tahadhari za kiafya ikiwa ni pamoja na kujifukiza

Leave a Comment