
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, Leo Juni 12, 2021 amezindua mtambo wa kisasa wa kupima na kutibu maradhi ya moyo katika Hospitali ya Jakaya Kikwete (The Jakaya Kikwete Cardiac Institute – JKCI).
“Nimeingia huko ndani na nimeona uchawi wanaoufanya kwa kweli kwa zamani ule ni uchawi, kwa sasa ni maeneleo ya teknolojia,”
Kuna mambo makubwa nimeona yanafanyika huko ndani, sasa hivi Tanzania tunajisifu sana kwa kupunguza sana vifo vya watoto, sasa hivi tuna watoto saba nadhani kwa vizazi 1000 hai,”

“Mwingine yupo ngazini hoi, kalala hapohapo ngazini lakini amelala anapumzika anasubiri alfajiri mapema kuna oparesheni nyingine zinaendelea, wanasema mcheza kwao hutunzwa, Serikali yenu itaangalia maslahi yenu,”
“Nimeoneshwa mpaka picha, madaktari wamefaya kazi usiku wamechoka, wamebanza kwenye pembe wamelala, sasa huyo aliyekwenda kuwapiga picha sijui ni nani lakini walistahiki kulala,”
“Nimefarijika kusikia pia kwamba miongoni mwa wanaotibiwa wanatoka nchi jirani, wanatoka Burundi, Comoro, Ethiopia, Malawi, Marekani wako hapa wamekuja na wametibiwa,”
“Sasa kuna ombi kwamba, wale wanaotibiwa kwa msamaha wa serikali, wangepelekwa nje au wangelipiwa hapa Jakaya Kikwete zingelipwa pesa hizi basi kati ya hizo angalau asilimia 50, 30 tugaieni tuendeleze huduma, nataka kumwambia waziri wa afya hilo liangalieni,” amesema Rais Samia
⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx