


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makallaleo June 21 amewaapisha Wakuu wapya wa Wilaya za Kigamboni na Ubungo walioteuliwa na Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan mwishoni mwa Wiki.
Wakuu wa Wilaya walioapishwa na RC Makalla ni pamoja na Kheri James alieyapishwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo pamoja na Mhe.Fatma Almass Nyangasa aliyeapishwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni.
Akizungumza wakati wa kuwaapisha Viongozi hao RC Makalla amewataka Viongozi hao kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao ipasavyo ikiwa ni pamoja na kusimamia ukusanyaji wa Mapato, kushughulikia kero za Wananchi, ulinzi na usalama, Usafi na usimamizi wa miradi ya maendeleo.