×

Mifugo Kuanza Kuvikwa Hereni

MWONGOZO wa utambuzi, usajili na ufuatiliaji wa mifugo kwa njia ya hereni za kieletroniki zinawekwa kwa mnyama mwenye umri zaidi ya miezi mitatu na kwamba zitasaidia pia kupunguza muingilianio wa mifugo kutoka maeneo mengine.

Hayo yamesemwa leo na Dk Audifas Sarimbo wa Idara ya Huduma za Mifugo kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi,katika utambulisho wa mwongozo wa utambuzi, usajili na ufuatiliaji wa mifugo kwa njia ya hereni za kieletroniki mkoani Simiyu.

Amesema pia zoezi hilo la uwekaji hereni za kieletroniki kwa mifugo linalofanyika kote nchini litamuwezesha mfugaji kuweza kupata mikopo kupitia taasisi mbalimbali za kifedha pamoja na kuikatia bima mifugo yake kwa kutumia namba za usajili zilizopo kwenye reheni ya mnyama.

Amesema hereni hizo pia zitasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza thamani ya ngozi ya mifugo ambayo imekuwa ikiharibiwa kwa kuwekewa alama kwenye ngozi kwa njia ya moto.

Zoezi la utambuzi, usajili na ufuatiliaji wa mifugo kwa njia ya hereni za kieletroniki linafanyika kwa mujibu wa sheria ya Mwaka 2011 ambapo linatekelezwa kwa mfugaji kulipia gharama ya shilingi 1,750 kwa ng’ombe na punda na shilingi 1,000 kwa mbuzi na kondoo.

Leave a Comment