UPDATES:
#UPDATES: Mashirika ya Ndege ya Uingereza yamepigwa marufuku kutua katika Viwanja vya Ndege vya Urusi pamoja na kupita kwenye Anga lake Uamuzi huo unafuatia uamuzi wa Uingereza kupiga marufuku Shirika la Ndege la Urusi, #Aeroflot kutua Nchini Uingereza.
Wakazi wa Ukraine Wapata Makazi Katika Vituo vya Treni
Wakazi wa Ukraine wamekimbilia vituo vya treni vya chini ya ardhi kuepuka mashambulio ya siku ya vikosi vya Urusi dhidi ya nchi yao.
Picha zinaonesha makundi ya wakazi na familia zao-wakiwemo watoto na wazee- wakilala katika vituo vya treni katika miji ya Kyiv na Kharkiv.
Wengi wao wamejifunika blanketi na kuvalia nguo za kuzuia baridi wakiwa wamezungukwa na begi zilizo na vitu vyao binafsi.

Amri ya kutotoka nje usiku mmoja iliwekwa nchini Ukrainia, na vituo vya metro viliendelea kuwa wazi ili kutumika kama vihifadhi vya mabomu.

Maelfu ya Waukraine wametoroka nyumba zao kutafuta usalama katika nchi jirani – takwimu ambayo Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Wakimbizi anakadiria kuwa zaidi ya 100,000.
Poland – ambayo inapakana moja kwa moja magharibi mwa Ukraine – pia imeanzisha vituo vya mapokezi kwenye mpaka wake ili kujiandaa kwa wimbi la wakimbizi wa vita.
Watanzania Wapo Salama Ukraine
Waziri wa Ukraine Atangaza vifo vya Raia 137 na Majeruhi 169


Mashirika Ya ndege Yaepuka Anga ya Ukraine
Picha hii inaonyesha hatua ya Urusi kuvamia Ukraine ilivyoathiri usafiri wa angani barani Ulaya huku mashirika ya ndege yakiepuka anga ya Ukraine wakati mzozo wake na Urusi ukizidi kufukuta.
Ukraine ilifunga anga yake kwa safari za ndege za kiraia saa za mapema baada ya Urusi kuanza mashambulizi yake.
Waziri wa Uchukuzi wa Uingereza Grant Shapps ameagiza Mamlaka ya Usafiri wa Anga kuhakikisha mashirika ya ndege yanaepuka anga ya Ukraine “kufuatia matukio ya kutisha usiku mmoja”.


