
Mataifa ya Sweden na Finland yamewasilisha rasmi maombi yake ya kujiunga na Jumuiya ya Kujihami (NATO) asubuhi ya leo Mei 18, 2022, Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg amesema “Ni kipindi cha kihistoria ambacho ni lazima tukitumie, uanachama wa ‘nchi za Scandnavia utaongeza usalama”.
Tangazo la Viongozi wa nchi hizo mbili kuhusu azma yao ya kuwasilisha maombi ya uanachama wa NATO limekuja kufuatia uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, Bunge la Sweden lilipiga kura kuunga mkono hatua hiyo, huku Finland ikifanya hivyo jana.
Finland inapakana na Urusi katika mipaka yake ya ardhini na nchi kavu, Finland na jirani yake Sweden ziliendelea kutounga mkono upande wowote katika kipindi chote cha vita baridi kwahiyo maombi yake ya kujiunga na NATO yanaonesha mabadiliko muhimu katika misimamo yake.
Mchakato wa kujiunga na NATO unaweza kuharakishwa na kuchukua wiki mbili tu, lakini utahitaji uungwaji mkono wa Wajumbe wote 30, uidhinishaji ambao unaweza kuchukua hadi mwaka mmoja.