×

Takribani Watu wapatao 18 Wamefariki kwa Kupigwa Risasi Nchini Madagascar

Polisi wakiwa tayari kukabiliana na waandamanaji Madagascar

POLISI nchini Madagascar walilazimika kutumia risasi ili kutawanya waandamanaji ambao walikua na gadhabu baada ya mtu mwenye ulemavu wa Ngozi kutekwa nyara.

 

Afisa wa polisi kutoka mji wa tukio wa Ikongo ulioko takriban kilomita 90 kusini mashariki mwa mji mkuu wa Antananarivo wakati akizungumza kwa njia ya simu na AFP amesema kwamba walijaribu kushauriana na waandamanaji hao , lakini pale walipokataa kusikia, hawakuwa na njia nyingine ila kutumia risasi za moto ili kujilinda.

 

Takriban watu 500 waliokuwa wamebeba visu na mapanga walijaribu kuingia kwa nguvu kwenye kituo cha polisi ambako washukiwa wa utekaji nyara walikuwa wameshikiliwa.

 

Mkuu wa polisi kitaifa Andry Rakotondrazaka amewaambia wanahabari kwamba tukio hilo ni la kuhuzunisha, na kwamba lingezuilika kama pangekua na maelewano kati yao na waandamanaji hao.

Mkuu wa Polisi nchini Madagascar

Kwa mujibu wa shirika la habari la nchini Madagascar limemnukuu Mganga mkuu wa hospitali iliyopo eneo a tukio Dr. Tango Oscar Toky. Katika ripoti yake amesema kwamba kati ya watu 34 waliojeruhiwa, 9 ni mahututi akiongeza kwamba wanasubiri helikopta za serikali ili kuwapeleka kwenye hospitali ya mji mkuu.

 

Imeandikwa: Dunstan Mtili Erick Kwa msaada wa mitandao

Leave a Comment