
Majina makubwa katika ulimwengu wa filamu na televisheni wamejitokeza kwa mbwembwe na mvuto mkubwa kwenye zulia jekundu la tuzo za Golden Globes za mwaka huu, hafla mojawapo ya heshima kubwa zaidi Hollywood inayofanyika jijini Los Angeles.
Zulia jekundu limekuwa kivutio kikuu, likijaa mavazi ya kifahari, mitindo ya kipekee na tabasamu kutoka kwa mastaa waliovutia macho ya mashabiki na wapiga picha duniani kote.

Mwanamuziki na mwigizaji Ariana Grande ameendelea kuthibitisha uimara wake katika tasnia ya filamu baada ya kuteuliwa kwa mwaka wa pili mfululizo kupitia filamu Wicked: For Good. Muonekano wake kwenye zulia jekundu ulikuwa miongoni mwa uliovuma zaidi usiku huo.
Kwa upande wake, Glen Powell, aliyewahi kung’ara katika filamu, ametambuliwa mwaka huu kupitia mfululizo wa vichekesho wa televisheni Chad Powers. Hili linaashiria mabadiliko makubwa katika safari yake ya kisanaa na kupokelewa vyema na mashabiki.
🎥 Filamu
Best Motion Picture – Drama: Hamnet
Best Motion Picture – Musical or Comedy: One Battle After Another
Best Director: Paul Thomas Anderson (One Battle After Another)
Best Original Score: Ludwig Göransson (Sinners)
Cinematic & Box Office Achievement: Sinners
Best Animated Film: KPop Demon Hunters
Uigizaji (Filamu)
Best Actress – Drama: Jessie Buckley (Hamnet)
Best Actor – Drama: Wagner Moura (The Secret Agent)
Best Actor – Musical/Comedy: Timothée Chalamet (Marty Supreme)
Best Actress – Musical/Comedy: Rose Byrne (If I Had Legs I’d Kick You)
Best Supporting Actress (Film): Teyana Taylor (One Battle After Another)
📺 Televisheni Yatinga Kwa Nguvu
Best TV Drama Series: The Pitt
Best TV Comedy Series: The Studio
Best Limited Series: Adolescence
🎬 Uigizaji (TV)
Best Actor – TV Drama: Noah Wyle (The Pitt)
Best Actor – TV Comedy: Seth Rogen (The Studio)
Best Actress – TV Drama: Rhea Seehorn (Pluribus)
Best Actress – TV Comedy: Jean Smart (Hacks)
Best Supporting Actor (TV): Owen Cooper (Adolescence)
🎤 Burudani Nyingine
Best Song: “Golden” – KPop Demon Hunters
Best Podcast: Good Hang With Amy Poehler
Best Stand-Up Comedy: Ricky Gervais – Mortality











