
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amewasili Chato Mkoani Geita, ambapo anatarajiwa kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mazishi ya Marehemu Bi. Suzana Magufuli ambaye ni Mama wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, yatakayofanyika tarehe 29 Mei 2026 Wilayani Chato.
Makamu wa Rais amepokelewa katika Uwanja wa Ndege Geita, Wilayani Chato, Mapokezi yaliyoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Martin Shigela, Viongozi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi pamoja na Viongozi mbalimbali Waandamizi.
Pia Makamu wa Rais, amefika nyumbani kwa marehemu, Kilimani Chato kusaini kitabu cha maombolezo pamoja na kuwafariji wafiwa kufuatia msiba huo.






