
Klabu ya Simba SC imetangaza rasmi kuachana na wachezaji saba ikiwa ni sehemu ya mchakato wa kuboresha kikosi kuelekea msimu mpya wa mashindano.
Kupitia kurasa zake rasmi za mitandao ya kijamii, Simba imewapongeza na kuwashukuru wachezaji hao kwa mchango wao walioutoa ndani ya klabu, huku ikiwatakia mafanikio mema katika hatua zinazofuata za maisha yao ya soka.
Wachezaji walioondoka ni:
- Chamou Karaboue
- Naby Camara
- Edwin Balua
- Joshua Mutale
- Awesu Awesu
- Omari Omari
- Moussa Camara
Hatua hiyo inaashiria mwanzo wa mabadiliko ndani ya kikosi cha Simba SC, huku uongozi wa klabu ukiendelea na mipango ya kukisuka upya kwa ajili ya msimu ujao.
Mashabiki wa Wekundu wa Msimbazi sasa wanasubiri kwa hamu kutangazwa kwa nyota wapya watakaojiunga na klabu hiyo katika dirisha la usajili ili kuimarisha kikosi kitakachowania mataji ya ndani na kimataifa.