×

Madeleka Atoa Msaada wa Milioni 1 Kwa Watoto wa Mjane – Video

Wakili Peter Madeleka.

Wakili Peter Madeleka ameguswa na changamoto ya mama mjane, Bi. Asha Baraka Saidi, anayeuguza watoto wake wawili wanaosumbuliwa na ugonjwa wa figo, taarifa zilizoibuliwa na Global TV.

Global TV iliripoti habari za mjane huyo mara kadhaa ambapo Watanzania walikuwa wakimsaidia kwa kidogo walichojaliwa ambapo Septemba 2, 2026, Madeleka ameonesha kuguswa na kumkabidhi mjane huyo kiasi cha shilingi milioni moja, fedha taslimu.

Aidha, ameitaka Serikali kuweka mkazo katika upatikanaji wa bima ya afya kwa wote, ili kila Mtanzania awe na uhakika wa kupata huduma bora za afya bila kujali hali yake ya kiuchumi.

Madeleka amesema Tanzania inahitaji kuweka vipaumbele vinavyogusa moja kwa moja maisha ya wananchi, akisisitiza kuwa taifa lenye watu wenye afya ndilo lenye uwezo wa kujenga uchumi imara na kusonga mbele.

Leave a Comment