×

PPRA Yatangaza Nafasi 10 za Ajira Katika Kada za TEHAMA

Dodoma, Septemba 1, 2026 — Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (PSRS), kwa niaba ya Public Procurement Regulatory Authority (PPRA), imetangaza nafasi 10 za ajira kwa Watanzania wenye sifa na uwezo unaohitajika.

Tangazo hilo lenye Kumb. Na. JA.9/16/01/54 limetolewa tarehe 1 Septemba 2026, likiwa na nafasi katika kada mbalimbali za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).

Nafasi zilizotangazwa

  1. ICT Officer II (Software Development – Frontend) — Nafasi 3
  2. ICT Officer II (Software Development – Backend) — Nafasi 4
  3. ICT Officer II (Artificial Intelligence Applications) — Nafasi 2
  4. ICT Officer II (Systems Analyst) — Nafasi 1

 

ICT Officer II – Software Development (Frontend)

Waombaji wa nafasi hizi wanatakiwa kuwa na Shahada ya Computer Science, Software Engineering, Information Technology, Information Systems, Computer Engineering au sifa inayolingana nayo kutoka taasisi inayotambuliwa.

Mwombaji anatakiwa kuwa na uzoefu wa vitendo katika miradi ya kutengeneza programu au portfolio inayoweza kuthibitisha uwezo wake. Pia anatakiwa kuwa na ujuzi wa Angular, TypeScript, HTML5, Tailwind CSS na teknolojia za kisasa za utengenezaji wa interfaces.

Aidha, anapaswa kuwa na ujuzi wa kutengeneza applications za simu kwa kutumia Flutter na Dart, kuunganisha mifumo na REST APIs na GraphQL, pamoja na kutumia Git, GitHub au GitLab.

Ujuzi wa UI/UX kwa kutumia Figma au zana nyingine zinazohusiana nao utakuwa faida ya ziada.

Mshahara: PPRA 5

ICT Officer II – Software Development (Backend)

Nafasi hizi zinahitaji mwombaji mwenye Shahada ya Computer Science, Software Engineering, Information Technology, Information Systems au Computer Engineering kutoka taasisi inayotambuliwa.

Mwombaji anatakiwa kuwa na ujuzi wa Java 21 au zaidi, Spring Boot, Spring Data JPA, Hibernate, REST APIs, GraphQL, PostgreSQL, RabbitMQ na mifumo ya asynchronous na event-driven architecture.

Ujuzi wa Kubernetes, Redis, Spring Security, OAuth2, JWT, JUnit 5, GraphiQL na Postman utakuwa faida ya ziada.

Mshahara: PPRA 5

ICT Officer II – Artificial Intelligence Applications

Waombaji wa nafasi hizi wanatakiwa kuwa na Shahada ya Computer Science, Software Engineering, Artificial Intelligence, Data Science au taaluma nyingine inayohusiana na teknolojia.

Mwombaji anatakiwa kuwa na ujuzi wa Python, TypeScript au JavaScript, pamoja na uzoefu katika AI execution pipelines, RESTful APIs, JSON na asynchronous programming.

Pia anatakiwa kuwa na uzoefu wa kutumia au kusanidi Large Language Models (LLMs) zinazoweza kuendeshwa ndani ya mifumo kama Ollama, LM Studio, vLLM au LocalAI, au kutumia huduma za LLM za mtandaoni kama OpenAI, Gemini au Anthropic.

Ujuzi wa prompt engineering, structured outputs, JSON schemas, function calling, tool use, agentic AI workflows, embeddings, vector databases na Retrieval-Augmented Generation (RAG) utahitajika kulingana na mahitaji ya nafasi.

Mshahara: PPRA 5

ICT Officer II – Systems Analyst

Nafasi hii inahitaji mwombaji mwenye Shahada ya Computer Science, Information Systems, Information Technology, Software Engineering, Computer Engineering, Business Information Systems au sifa inayolingana nayo.

Mwombaji anatakiwa kuwa na uelewa au uzoefu wa vitendo katika systems analysis, enterprise information systems, user requirements gathering, system testing, ICT user support, business process analysis na technical documentation.

Ujuzi katika cybersecurity, enterprise applications na Government ICT systems utakuwa faida ya ziada.

Mshahara: PPRA 5

Masharti muhimu ya maombi

PSRS imesema waombaji wote lazima wawe raia wa Tanzania na wasizidi umri wa miaka 45.

Waombaji wanatakiwa kuambatanisha nakala zilizothibitishwa za vyeti vyao vya elimu na taaluma, transcripts, vyeti vya usajili wa kitaaluma pale inapohitajika, pamoja na cheti cha kuzaliwa.

Aidha, Form IV na Form VI result slips, testimonials na partial transcripts hazitakubalika.

Mwombaji anatakiwa pia kupakia picha ya Passport Size ya hivi karibuni katika Recruitment Portal na kutaja referees watatu wenye mawasiliano yanayoaminika.

Waombaji wenye vyeti vya elimu vya nje ya Tanzania wanatakiwa kuhakikisha vyeti hivyo vimetambuliwa na mamlaka husika, ikiwemo TCU, NECTA au NACTVET.

Jinsi ya kutuma maombi

Maombi yote yanatakiwa kuwasilishwa kupitia Recruitment Portal ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.

Recruitment Portal: portal.ajira.go.tz

Barua ya maombi inapaswa kuandikwa kwa Kiswahili au Kiingereza, kusainiwa na kuelekezwa kwa:

Secretary,
President’s Office, Public Service Recruitment Secretariat,
P.O. Box 2320,
Mahakama Street, Tambukareli,
Dodoma.

Mwisho wa kutuma maombi

Mwisho wa kutuma maombi ni Septemba 14, 2026.

PSRS imesema ni waombaji watakaoteuliwa pekee ndio watakaofahamishwa kuhusu tarehe ya usaili.

Aidha, mwombaji atakayewasilisha vyeti vya kughushi au taarifa za uongo atachukuliwa hatua za kisheria.

Maombi yatakayowasilishwa kupitia njia nyingine tofauti na Recruitment Portal hayatazingatiwa.

Chanzo: Public Service Recruitment Secretariat (PSRS), Tangazo Kumb. Na. JA.9/16/01/54, Septemba 1, 2026.

Leave a Comment