
Rais wa Marekani, Donald Trump, amemjibu rais wa zamani wa Marekani, Barack Obama, kufuatia kauli ya Obama kwamba dunia inaweza kuwa katika hali nzuri zaidi iwapo wanawake wangepewa nafasi ya kuongoza serikali zote duniani kwa kipindi cha miaka miwili.
Obama alitoa kauli hiyo Septemba 21, 2026, wakati wa mazungumzo na mwanahistoria Doris Kearns Goodwin katika Chuo Kikuu cha Salem State, Massachusetts.
Katika mazungumzo hayo, Obama alisema kuwa iwapo wanawake wangepewa nafasi ya kuongoza serikali zote kwa miaka miwili, mambo yasingekuwa kamilifu, lakini anaamini hali ingeweza kuwa bora zaidi.
Kauli hiyo imejibiwa na Trump wakati akizungumza na waandishi wa habari nje ya Ikulu ya Marekani.
Trump amesema anawapenda wanawake na kuwaona kuwa wazuri, lakini amelikataa wazo hilo la Obama, akilitaja kuwa ni kauli ya “kipuuzi.”
Mjadala huo umeibuka wakati viongozi hao wawili wakiendelea kuwa na mitazamo tofauti kuhusu uongozi na namna serikali zinavyopaswa kuendeshwa.
Stori na Tereza Muga | GPL -TUDACO