
LOS ANGELES: Mwanamuziki na nyota wa vipindi vya televisheni, Pauly D, amemvisha pete ya uchumba mpenzi wake wa muda mrefu, Nikki Hall, baada ya kuwa katika uhusiano kwa miaka sita.
Pauly D na Nikki Hall walianza uhusiano rasmi mwaka 2020, baada ya kukutana katika kipindi maarufu cha televisheni cha MTV, Double Shot at Love.

Akizungumzia hatua hiyo, Nikki amesema alifurahi kupokea ombi la Pauly D, akieleza kuwa kwa miaka yote hiyo wamekuwa wakichaguana, kujenga maisha pamoja na kufurahia safari yao ya kimapenzi.
Habari za uchumba huo zimepokelewa kwa hisia mbalimbali na mastaa wenzao wa kipindi cha Jersey Shore.

Rafiki yake wa karibu, Vinny Guadagnino, alitoa pongezi zake kwa njia ya utani, akitumia video iliyotengenezwa kwa teknolojia ya AI iliyoonyesha akilia kwa furaha kufuatia taarifa hizo.
Uchumba huo sasa umefungua ukurasa mpya katika uhusiano wa Pauly D na Nikki Hall, huku wawili hao wakielekea katika hatua ya ndoa baada ya miaka kadhaa ya kuwa pamoja.
Stori na Hasina Thabit | GPL -TUDACO