×

Dyna: Nimeacha Kujichubua

Dayna Nyange

Na JOHN JOSEPH| CHAMPION IJUMAA| MAKALA

JINA lake halisi ni Mwanaisha Nyange lakini jina la biashara ni Dayna Nyange, staa wa Bongo Fleva ambaye kwa sasa anatamba kupitia wimbo wake wa Komela aliomshirikisha Bill Nas. Mdada huyo mrembo, mwembamba ambaye alianza kupata umaarufu miaka kadhaa iliyopita, amezungumza na Championi Ijumaa katika maho jiano maalum na kufunguka mambo mengi kuhusu maisha yake binafsi.

Dayna Nyange

Dayna alianza kutamba na wimbo wa Mafungu akimshirikisha Marlaw, baada ya hapo akaendelea kutoa nyingine kadhaa zikiwemo Nivute Kwako akiwa na Barnaba na I Do.

Kwa sasa makazi yake yapo jijini Dar. Inawezekana moja kati ya maswali aliyoulizwa hapa umekuwa ukitamani kumuuliza, sasa nafasi yako hii, burudika:

WEWE NI MAMA, MWANAO ANAITWA NANI NA ANA UMRI GANI? Anaitwa Rahma na ana miaka 10, naishi  mitandao ya kijamii.

RAHMA ANAMJUA SHEMEJI YETU WA SASA?

Sipendi mwanangu ajue mambo yangu binafsi, hamjui na siwezi kumuonyesha boyfriend wangu, nitamuonyesha mume wangu.
TUELEZEE KUHUSU SHEMEJI YETU ULIYENAYE SASA.

Dayna Nyange

Nipo kwenye uhusiano lakini ambao haueleweki kwa kweli, kwa ufupi ni ‘complicated’ lakini siwezi kufunguka zaidi kwa kuwa sipendi maisha yangu binafsi kuyaanika hadharani.
UNA MPANGO WA KUTAFUTA MDOGO WA RAHMA MWAKA HUU?

Ikiwezekana inaweza kuwa hivyo, kuna muda natamani kuwa na mtoto lakini bado sijapata mtu sahihi.
MBONA WEUPE WAKO UMEPUNGUA, UMEACHA KUJICHUKUA?

(Anacheka, anajitazama mikononi)

Ndiyo nimeacha, japo ngozi yangu haijabadilika kiasi hicho.
CHANZO CHA KUJICHUBUA ILIKUWA NI NINI NA KWA NINI UMEACHA?

Ilianza kama utani, kuna mafuta nilitumia yakanifanya niwe mweupe, nikajikuta naendelea kuyapaka, ilivyokuwa ikizungumzwa na wengi nikaona ni sawa tu. Kuna muda nilijichubua mpaka nikawa naona mishipa yangu inatokeza. Kuna watu wengi hawakufurahishwa na mimi kujichubua, walikuwa wananiambia, mmoja wao ni Fid Q, baadaye niliamua tu mwenyewe kuacha. Nadhani sababu za kuingia huko ni ujana tu.
MAMA YAKO ALIZUNGUMZIAJE KUJICHUBUA KWAKO?

Katika makuzi yangu sikuwa karibu na mama, hivyo hakuwa mzungumzaji sana, ila nilipokuwa nikionana naye aliniambia kuwa siyo vizuri. Pia wakati nimejichubua sikuwa karibu na ndugu zangu wengi.

UMEWAHI KUWA NA UHUSIANO NA MBONGO FLEVA?

Sijawahi na wala sitaki.

KWA NINI?

Sipendi tu lakini labda hawajui kutongoza, unajua sisi wanawake tunajifunza kupenda, nyie wanaume ndiyo mnapenda, sasa unaweza kusema sitaki lakini ukikutana na mtaalam wa kutongoza unaingia kwenye mstari wewe mwenyewe. Ningetembea na msanii wa Bongo Fleva ingejulikana tu, hawanaga siri hao.

HIVI UNA UMRI WA MIAKA MINGAPI?

Hapana, hilo liache kwanza.
UNAZUNGUMZA KIKABILA GANI?

Sijui sana lugha za makabila labda kidogo Kirangi na Kigogo.

ASANTE MAMA RAHMA KWA MUDA WAKO.

Ah ah ah acha zako wewe

 

Kwa stori zote kali, Tu-follow

Facebook @Globalpublishers

Twitter @GlobalHabari

Instagram @GlobalPublishers

YouTube @GlobalTVTZ