×

Ngoma Kurejea Yanga Jumamosi

Na Khadija Mngwai| Championi Jumatano | Habari

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Yanga, Donald Ngoma raia wa Zimbabwe, anatarajia kurejea katika kikosi chake hicho mwisho mwa wiki hii akitokea nchini Afrika Kusini alipokwenda kufanyiwa matibabu.

Ngoma aliondoka kikosini hapo hivi karibuni bila ya kuuaga uongozi wake ambapo akielezwa kuwa amekwenda kufanya matibabu ya goti nchini Afrika Kusini ambapo anakaribia wiki mbili hadi sasa.

Akizungumza na Championi Jumatano, Meneja wa Yanga, Hafidh Salehe amesema kuwa mchezaji huyo yupo mbioni kurejea klabuni hapo baada ya hali yake kutengemaa tayari kujiunga na wenzake kwa ajili ya kutetea ubingwa wa ligi kuu.

“Ngoma anatarajia kurejea nchini siku ya Jumamosi na ameshatoa taarifa kwa uongozi juu ya kurejea kwake na hali yake inaendelea vyema kwa ajili ya kuendelea na mbio za kuwania ubingwa wa ligi kuu.

“Lengo letu ni kuona timu yetu inafanikiwa kutwaa ubingwa msimu huu hivyo ujio wake utasaidia kuongeza nguvu katika kikosi hicho kuhakikisha tunafanikiwa kushinda mechi zote zilizobakia,” alisema Hafidh.

Leave a Comment