




MKURUGENZI wa Taasisi ya Tulia Trust na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, leo amezindua mashindano ya baiskeli na mbio zinazotarajiwa kufanyika Mei 6, mwaka kuu katika Viwanja vya Sokoine mkoani Mbeya.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati akizundua mashindano hayo, Dkt. Tulia amesema kuwa kutakuwa na mbio ndefu za kilomita 42, ambapo katika mbio hizo mshiriki atalipia elfu 30, mbio fupi ‘half marathon’ km 21 shilingi elfu 20 na kwa upande wa waendesha baiskeli km 1500 kwa wanaume na wanawake Km 75 ni shilingi elfu 20.
Kwa mshiriki ambaye ni raia wa nje atalipia dola elfu 20 ili aweze kuwa miongoni mwa washiriki. Pia kuna mbio fupi za ndani ya uwanja mita 100, mita 200, mita 400, mita 800, mita 1500 ambazo kiingilio chake ni elfu kumi.
Pia kutakuwa na mbio za watoto km 2 na wazee, km 2 kwa walemavu na km 5 kwa wanafunzi wa vyuo na sekondari ambao hawana viingilio, badala yeke watatakiwa kuja na vitambulisho kwa wanachuo na nguo maalum za michezo kwa wanafunzi wa sekondari. Vilevile watajipatia zawadi kwa washindi watakayeibuka kidedea katika mashindano hayo.
Aidha mshindi wa kwanza wa Km 42 atapata mil 3, baiskel mil 2, km 21 mil 2 ambapo mshiriki ili ajisajili anapaswa kuingia tovuti ya www.tuliatrust.org
Fedha ambazo zitapatikana katika mashindano hayo zitaelekezwa katika kusaidia masuala ya kijamii kama vile elimu na afya.
NA DENIS MTIMA/GPL.