×

Uchafu Dar: Zungu Amnyamazisha Mdee, Amwambia “Kaa Chini” – Video

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mussa Zungu, amesema dampo linalotumiwa na Jiji la Dar es Salaam lililopo Pugu Kinyamwezi lina hali mbaya.

Zungu ameyasema hayo leo Alhamisi Januari 30, 2020 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Kawe, (Chadema), Halima Mdee.

 

Halima ametaka kufahamu Serikali ina mpango gani wa kujenga dampo la kisasa jijini Dar es Salaam ili kutatua changamoto ya uchafu.

 

“Je Serikali ina mpango gani wa kujenga dampo la kisasa kwenye maeneo mengine kila wilaya ili kuzuia uchafu kutokana na lililopo kutokidhi kubeba uchafu katika jiji zima?” amehoji.

 

Akijibu swali hilo, Zungu amesema kasi ya taka katika jiji hilo ni kubwa licha ya kwamba linakua kwa kasi na kwamba miaka ijayo linakadiriwa kuwa na watu zaidi ya milioni nane hadi tisa na dampo ni moja.

 

“Ni kweli hali ni ya uchafu na mbaya lakini nimwondoe hofu mbunge kuwa fedha zipo zimeshatolewa ili kujengwa dampo la kisasa jipya ambalo litabeba taka zote katika jiji la Dar es Salaam,” amesema.

Leave a Comment