KATIKA hali ya kushangaza, Warembo wamemiminika katika ibada ya maombezi iliyofanywa na Kiongozi wa Kanisa la Ufunuo, Askofu Paul Bendera juzi Jumapili katika Kanisa hilo lilolopo Kimara Bonyokwa jijini Dar es Salaam.
Mbali na warembo hao, pia wanawake ambao wako kwenye ndoa na hawajapata watoto kwa muda mrefu na wanatamani kuzaa, walifika kwa ajili ya maombezi ili waweze kupokea miujiza ya Mungu.
Licha ya maombi hayo, Nabii Bendera aliwartabiria wanawake hao kuwa mpaka mwakani mwezi machi watakuwa wamepata watoto huku akiwatabiria warembo hao kuapata wanaume ambao watakuwa ni hitaji lao la moyo na wataishi nao katika maisha yao ya ndoa.
