RAIS wa Marekani, Donald Trump, amesema kauli yake ya kuwazuia watu kutoka Bara la Ulaya kuingia Marekani haikupaswa kusubiri hadi aongee na viongozi wote wa Ulaya kwa sababu ni suala la dharura lililopaswa kufanywa kwa haraka.
”Uingereza wanafanya kazi nzuri wanadhibiti virusi vya Corona, ndiyo maana sijawazuia,” amesema Trump.”
Viongozi wa Umoja wa Ulaya wamekosoa vikali uamuzi wa Marekani kupiga marufuku watu wanaotoka Ulaya kuingia Marekani, huku wakisema janga la virusi vya Corona ni mgogoro wa dunia sio wa bara moja tu huku wakishangaa Trump kufanya maamuzi bila kuwashirikisha.
Trump amepiga marufuku watu wanaotokea nchi zote za Bara la Ulaya (isipokuwa Uingereza) kuingia Marekani ili kuzuia kuenea kwa virusi Corona.
View this post on Instagram
