AMA kweli wanasema hayawi hayawi sasa yamekuwa! Ile promosheni namba moja kwa sasa hapa Tanzania ya bahati nasibu ya Chomoka na Gari mpya aina ya Totoya FunCarge inayoendeshwa na magazeti bora ya michezo , Championi na SpotXtra tayari imezinduliwa jijini Mwanza.
Timu ya masoko Kanda ya Ziwa ikiongozwa na afisa wake Khamis Kikasi juzi Jumatatu ilitinga jijini Mwanza kuzindua rasmi Chomoka na Gari Mpya na kushangazwa na mapokeo makubwa ya promosheni hiyo kutokana na wasomaji wa magazeti ya michezo nchini kujitokeza kwa wingi ambapo wengi wao walichangamkia magazeti yaliyokuwa yakiuzwa huku mamia wakijaza kuponi maalumu kwa ajili ya kutaka kujishindia gari mpya.
Timu ya masoko ilitembelea maeneo mbalimbali ya Jiji la Mwanza ikiwemo, Pasiansi, Kona ya Bwiru, Igoma, Mecco, Buzuruga, Mabatini, Mwanza mjini , Mkuyuni, Nyegezi Kona, Nyegezi Stand, Mkolani na mji unaokuwa kwa kasi wa Buhongwa ambapo baada ya promosheni hii kabambe kuingia katika mji huo watu walitanda barabarani wakionekana kufuatilia kwa umakini promosheni hiyo.
Wasomaji wa magaeti hayo waliya changamkia na kujaza kuponi zilizowawezesha kuingia kwenye kinyang’anyiro cha kushinda Gari Mpya huku wakiahidi kununua magazeti hayo zaidi na zaidi ili waweze kushiriki bahati nasihu hiyo kikamilifu na waweze kupata bahati ya kujishindia ndinga hiyo mpya.
Hii ni wiki ya nne tangu kampuni ya Global Publishers ilipozindua bahati nasibu hiyo kupitia magazeti ya Championi na Spoti Xtra ambapo wasomaji watakaonunua magazeti hayo kwa wingi wataweza kunufaika na ushindi wa gari mpya aina ya Toyota FunCargo. Mbali nna zawadi hiyo, kila washindi 10 wataondoka na Simu Janja mpya za mikononi aina ya Smart Kitochi zikiwa zimesheheni bando la bure na App ya Global ambayo ndani ina +255 Global Radio na TV Online.
JINSI YA KUSHIRIKI
Nunua gazeti la Championi na Spoti Xtra kisha fungua ukurasa wa pili ambapo utakutana na kuponi yenye maelekezo ya kushiriki bahati nasibu hiyo kwa kujaza kuponi kama maelekezo yalivyo.
JINSI YA KUTUMA
Mpe kuponi muuza magazeti aliye karibu yako au peleka kwenye ofisi za Global Publishers zilizopo Sinza-Mori Dar es Salaam au tuma kwa njia ya barua kwa Jishindie Gari, Global Publishers S.L.P 7534 Dar es Salaam. Kwa maelekezo zaidi piga simu namba 0717020792 au 0672324759.
MASHARTI YA USHIRIKI
Wafanyakazi wa kampuni ya Global Publishers & General Enterprices Ltd na watoto wa umri chini ya miaka 18 hawaruhusisi kushiriki bahati nasibu hii. Kuponi zitumwe kutoka nakala halisi, vivuli (fotokopi) haviruhusiwi. Mtu anaruhusiwa kutuma kuponi nyingi kadri awezavyo ili ajiongezee nafasi ya kushinda. Kuponi zote zitachezeshwa kwenye droo ya awamu ya kwanza, ya pili na ya tatu.
Na Johnson James, Mwanza




