×

Uingereza Yajitoa Rasmi Umoja wa Ulaya

UINGEREZA imeanza ukurasa mpya wa kujitegemea kwa kujitoa katika Umoja wa Ulaya (EU), baada ya usiku wa kuamkia jana kukamilisha rasmi safari hiyo.

 

Uingereza iliacha kufuata sheria za EU kuanzia saa sita usiku kuamkia Ijumaa, ambapo sasa itakuwa na sheria zake za kusafiri, biashara, uhamiaji na usalama.

 

Waziri mkuu wa Uingereza, Boris Johnson, amesema “uhuru uko mikononi mwao” na kuwa na uwezo wa “kufanya vitu tofauti na kwa namna bora”, akisema mchakato wa muda mrefu wa kujitoa umekamilika.

 

Licha ya hatua hii, wanasiasa na watu waliopinga nchi hiyo kujitoa EU, wanasema hali itakuwa mbaya zaidi.

 

Waziri wa Scotland,  Sturgeon, ambaye mara zote amekuwa akitaka nchi yake kubaki EU, amesema kupitia ukurasa wake wa kijamii wa twitter “Scotland itarejea karibuni kwenye umoja wa Ulaya, kuweni na imani”.

 

Mawaziri wa Uingereza, wameonya kuhusu uwezekano wa kushuhudiwa sintofahamu katika baadhi ya mambo, wakati huu taifa hilo likitekeleza sheria zake tofauti na zile za EU.

Leave a Comment