×

JPM Achafukwa, Amwambia Rostam: Gombea Ubunge Umtoe Abood – Video

RAIS John Magufuli amemwomba aliyewahi kuwa mbunge wa wa jimbo la Igunga na mfanyabiashara maarufu nchini, Rostam Abdulrasul Aziz, kugombea Ubunge katika jimbo la Morogoro Mjini ili kumtoa Mbunge wa sasa, Abdul-Aziz Mohamed Abood baada ya mbunge huyo kushindwa kuendeleza viwanda viwili alivyopewa na serikali kwa miaka 24.

 

 

Amesema hayo leo Ijumaa, Februari 12, 2021 wakati akizindua kiwanda cha ngozi cha Ace Leather Ltd, Morogoro alichokuwa amepewa Abdul-Aziz Abood na sasa anakimiliki Rostam.

 

 

“Unapokuwa na kiwanda ni utajiri, hautouza malighafi nje, ukisafirisha malighafi ni sawasawa na kuuza ajira, leo nimefurahi, hongera Rostam kwa kuanzisha kiwanda hiki, endeleza hiki kiwanda.

 

 

“Nampenda sana Abood na jana nilimpongeza ila kwenye hili la kukaa na viwanda viwili kwa miaka 24 bila kuviendeleza, imeniuma sana, bora Rostam ulikaa nacho wee hiki kiwanda ila leo umekiendeleza, ila Abood alikaa navyo wee, akakopea pesa akanunua magari.

 

 

“Rostam nakupongeza umefanya yaliyo mema, nilifikiria siku nyingine uje ugombee ubunge hapa Morogoro umtoe Abood aliyewakosesha ajira wapiga kura wake iwe fundisho, kukaa na viwanda viwili kwa miaka 24 bila kuviendeleza, Abood kwa miaka hii mitano jenga kiwanda.

 

 

“Rostam nakupongeza sana kwa kiwanda hiki, kwa sababu ndugu yako Mbunge wa hapa Abood alichukua viwanda viwili na akashindwa kuviendeleza tangu 1996 hadi mwaka jana aliponyang’anywa, huenda wengine walikufa kwa kukosa ajira na akawabeba kwenye mabasi yake kwenda kuwazika,” amesema Magufuli.

 

Leave a Comment