×

Fahyma, Paula Mwisho wa Ubishi

WAREMBO wawili maarufu Bongo wanaozungumzwa zaidi juu ya ni nani anayejua kuvaa kuliko mwingine,
Fahyma na Paula Kajala;
ubishi huo unakwenda kufikia mwisho ‘soon’.


Fahyma ambaye ni
baby mama wa msanii Rayvanny aliyeporwa tonge kinywani na Paula; wawili hao wanawania
tuzo kwenye Kipengele
cha Female Stylish Personaliy of the Year 2021 kupitia Tuzo za Swahili Fashion Week
zitakazofanyika Serena
Hotel jijini Dar kati ya Desemba 3 hadi 5, 2021.


Pamoja na kwamba
kuna wengine wakali kama Hamisa Mobeto na Jokate Mwegelo, lakini ushindani mkubwa unatajwa kuwa kwa Fahyma na Paula kutokana na kile kinachoendelea kati yao; kudaiwa ‘kushea’ mwanaume ambaye ni Rayvanny.

STORI; MWANDISHI WETU, DAR

Leave a Comment