×

Bilionea Namba moja Duniani Aja Na Balaa Jipya, Aanzisha Mji Wake Mpya – Video

Bilionea Namba moja Duniani, Elon Musk, ambaye kwa sasa ndye Bilionea wa kwanza aliyefikisha utajiri wa zaidi ya dola BILIONI 400, ameibuka na jambo lingine kubwa zaidi – anajenga mji wake, huko Texas Nchini Marekani.

Je, hii imekaaje? Tuogope au tushangilie kwa maajabu haya anayoyafanya Bilionea huyu ambaye yeye na Rais mteule wa Donald trump ni marafiki wa dam dam?

Wafanyakazi wa SpaceX wamewasilisha ombi rasmi la kuanzisha mji wa Elon Musk utakaojulikana kwa jina la Starbase, ambapo meya wa kwanza wa mji huo anapendekezwa kuwa msimamizi wa usalama wa kampuni hiyo.

Kwa miaka kadhaa, Elon Musk amepanua shughuli zake Texas, akihamisha makampuni yake kutoka California na kujenga ofisi, maghala, na viwanda katika kaunti kadhaa za Texas zinazozidi kuongezeka.

Leave a Comment