×

Yule askofu anaswa gesti

Stori: Issa Mnally na Richard Bukos, IJUMAA
DAR ES SALAAM: Yametimia! Yule Askofu wa Kanisa la Jesus Deliverance Center (JDC) lililopo Tabata- Matumbi jijini Dar, Derik Mathias (pichani) amenaswa na makamanda wa kikosi maalum cha Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ cha Global Publishes akiwa katika maandalizi ya kuivunja Amri ya 6 ya Muumba.

Askofu huyo alinaswa katika nyumba ya kulala wageni ‘gesti’ iliyopo Ubungo- Kibangu, Dar akiwa chumbani na binti wa miaka 16 ambaye ni mtoto wa mzee wa kanisa lake (jina kapuni).

ALISHAPEWA ONYO
Tukio hilo limekuja ikiwa ni siku kadhaa baada ya habari yake kuandikwa kwenye gazeti hili toleo lililopita ikiwa na kichwa; ASKOFU AMUOMBA PENZI MTOTO WA MZEE WA KANISA.
Sasa juzi, makamanda wa OFM wakiwa katika ubora wao wakitafuta matukio, mtu mmoja alipiga simu akisema askofu huyo hakukoma, aliendelea kumhadaa binti huyo.

KILICHOTOKEA
“Sasa leo wanakutana gesti ya….(anaitaja jina), ipo pale Tabata Matumbi. Kwa hiyo nyie OFM kwa sababu mlishampa onyo kuachana na binti huyo lakini hajakoma, hebu ibukeni muda huo mkaone mambo,” alisema mtu huyo aliyepiga simu.

SAA 3 USIKU
Makamanda wa OFM waliendelea na harakati zao za kusaka matukio, lakini ilipofika saa 2:30 usiku, walipigiwa simu na yule mtu wakiambiwa kuwa, tayari askofu na binti huyo wamezama chumbani kwenye gesti hiyo lakini nje ya gesti kuna watu kibao ambao ni madereva wanaolala hapo wakitokea mikoani.

OFM YATINGA, HALI TETE
Ndani ya dakika ‘sifuri’ OFM waliwasili kwenye gesti hiyo tayari wakiwa na polisi ambapo kweli waliwakuta wateja kibao wakibadilishana mawazo kwa sauti za juu hivyo kuondoa hata ile maana ya ‘nyumba ya kulala wageni’!!

KIZUIZI NAMBA MOJA
Polisi hao walijieleza mbele ya watu hao na mhudumu wa gesti ambaye alimwita mmiliki wake aliyetafsirika kwa sauti na umbo kwamba ni mwenyeji wa kutoka Mkoa wa Iringa kama si Njombe.

KIZUIZI NAMBA MBILI
Baada ya kuwasili kwa mmliki huyo, bado uwezekano wa kuingia ndani ya gesti kwenye chumba alicho ‘baba askofu’ na binti huyo ukawa haupo baada ya bosi huyo akisaidiwa na wateja wengine ambao pia walionekana kutoka mkoa mmoja, kugoma katakata wakisema askofu huyo ni mteja wa hapo hivyo hawezi kuacha aumbuke.

“Hata kama nyie ni polisi lakini mimi askofu ni mteja wangu. Sasa nikisema niwaruhusu muingie ili mkamkamate sitakuwa natenda haki. Hapa haingii mtu,” alisema mmiliki huyo.

NGUVU YATUMIKA
Ilibidi polisi hao kutumia nguvu ya kikazi kuingia ndani ambapo na OFM nao kwa kutumia mwanya huo, walizama ndani ya chumba na kumkuta ‘baba askofu’ huyo akiwa ndani ya bukta ya bluu ya maji ya bahari huku binti akionekana kutokwa jasho!

Binti huyo alisema jasho lake lilitokana na kukuru kakara ya hapa na pale ndani ya chumba hicho ambapo askofu huyo alikuwa kwenye muhemko.

OFM ANYANG’ANYWA KAMERA
Hata hivyo, baada ya wapiga picha wa OFM kumchapa za kutosha askofu huyo, mmoja kati ya watu waliokuwa wakitia ngumu, alimnyang’anya kamera mpiga picha mmoja wa OFM ambapo polisi walitumia nguvu nyingi kuirejesha kamera hiyo kwa mhusika.

ASKOFU ATABIRI CHUMBANI
Kufuatia kitendo hicho, baba askofu alisikika akimwambia binti huyo maneno haya:
“We binti naamini unahusika katika hili tukio la kuvamiwa hapa. Lakini sikulaumu wewe kwani ni Mungu amekutumia ufanye hivi ili mimi nijirekebishe.” Kauli hiyo iliwavunja mbavu polisi huku OFM wakiwa wamenuna!

Baada ya hapo, askofu, binti na polisi hao waliingia ndani ya gari kuelekea kituoni kwa hatua nyingine huku OFM wakirudi mitaani kuendelea kusaka matukio! Hapa Kazi Tui!

Leave a Comment