×

TLS Yataka Ufafanuzi wa Kisheria Kuhusu Agizo la Polisi 2025 – Video

Tanganyika Law Society (TLS) imesema moja ya mambo ambayo Watanzania walitarajia kupata ufafanuzi katika ripoti ya Tume ya Uchunguzi wa matukio ya uvunjifu wa amani kabla na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 ni uhalali wa agizo lililotolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi, Camillus Wambura.

Katika agizo hilo, IGP Wambura aliwataka wakazi wa Dar es Salaam kutotoka nje ya makazi yao huku Jeshi la Polisi likiendesha doria katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya kulinda usalama.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Jumatatu Mei 11, 2026, Rais wa TLS, Boniface Mwabukusi, amesema kutokana na uzito wa suala hilo katika muktadha wa sheria na Katiba, umma ulikuwa unatarajia tume hiyo kulizungumzia kwa kina.

Mwabukusi amesema taarifa iliyowasilishwa na Mohamed Chande Othman haikutoa maelezo yoyote kuhusu uhalali wa agizo hilo wala athari zake kwa haki za kiraia na utawala wa sheria.

“Tume haikugusia kabisa jambo hili,” amesema Mwabukusi.

Kauli hiyo ya TLS imekuja wakati mijadala kuhusu haki za kiraia, usalama na utekelezaji wa sheria ikiendelea kujitokeza kufuatia matukio yaliyozunguka uchaguzi mkuu uliopita.

Leave a Comment