×

RC Chalamila Aagiza Gereji Pembezoni mwa Barabara Dar Ziondolewe

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, ameagiza kuondolewa kwa gereji zote zilizo pembezoni mwa barabara kuu ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam ili kuboresha usalama wa watumiaji wa barabara na kuimarisha mpangilio wa jiji.

Akizungumza leo Juni 15, 2026 katika mkutano na wenyeviti wa serikali za mitaa uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Chalamila amesema uwepo wa gereji hizo kando ya barabara kuu umekuwa ukisababisha usumbufu wa usafiri, kuongeza hatari ya ajali, na kuathiri usafi pamoja na muonekano wa jiji.

Ameeleza kuwa mamlaka husika zinapaswa kuhakikisha gereji zote zilizojengwa au zinazofanya shughuli pembezoni mwa barabara kuu zinaondolewa kwa kufuata sheria, taratibu na maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya shughuli hizo.

Hatua hiyo imeelezwa kuwa sehemu ya juhudi za serikali za kuboresha mipango miji, kuongeza usalama barabarani na kufanya Dar es Salaam kuwa jiji lenye mpangilio bora zaidi na mazingira safi kwa wakazi wake na watumiaji wa barabara.

Leave a Comment