×

Mke wa Rais Korea Kusini Atupwa Jela Miaka 7 Kwa Makosa ya Rushwa

Mahakama ya Wilaya ya Seoul Nchini Korea Kusini imemhukumu Kim Keon Hee, Mke wa Rais wa zamani Yoon Suk Yeol, kifungo cha miaka saba jela baada ya kupatikana na hatia ya kupokea rushwa ya zawadi za kifahari kwa ajili ya upendeleo wa kisiasa.

Katika kesi hiyo imebainika kuwa Kim amepokea zawadi mbalimbali za thamani kubwa zikiwemo vito vya dhahabu, mkufu wa Van Cleef & Arpels, brooch ya Tiffany, pete za Graff, begi la Dior, pamoja na saa ya Vacheron Constantin na mchoro wa thamani kubwa.

Aidha, Mahakama imesema zawadi hizo zimetolewa na Watu mbalimbali waliokuwa wakitafuta upendeleo wa kisiasa na nafasi za juu serikalini kupitia ushawishi wake kama Mke wa Rais, hali iliyotajwa kuharibu imani ya umma kwenye mfumo wa Uongozi.

Katika huku hiyo, ilibainishwa kuwa Kim ametumia nafasi yake kushawishi upatikanaji wa ajira na fursa za Serikali kwa Watu waliompa zawadi hizo, jambo lililoathiri uwazi na usawa katika utendaji wa Serikali.

Hata hivyo, Kim amekanusha mashtaka hayo na kupitia Mawakili wake na ameeleza kuwa atakata rufaa dhidi ya hukumu hiyo, wakati akiwa tayari anakabiliwa na kesi nyingine zinazohusiana na rushwa na udanganyifu wa kifedha.

Leave a Comment