Madalali wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) wamefika katika ofisi za gazeti la Tanzania Daima zilizopo jengo la Klabu maarufu jijini Dar, Bilicanasa, leo asubuhi na kuanza kuondoa vifaa ofisini hizo kutokana na deni la pango la mmiliki wa gazeti hilo, Freeman Mbowe.
Mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima, Neville Meena amethibitisha hayo na kusema kuwa kwa sasa wako kwenye msukosuko mkubwa lakini wanafanya jitihada za kukabiliana na hali hiyo ili kuhakikisha uzalishaji wa gazeti unafanyika kama kawaida.
Siku za hivi kaibuni, Mkurugenzi wa NHC, Bw. Nehemia Mchechu alimtaja Mbowe kama miongoni mwa wadaiwa sugu wa shirika hilo na kudai alishamuandikia notisi yakulipa deni notisi ambayo imeisha jana.
Inasemekana pia kuwa, Klabu ya Bilicanas nayo ipo hatarini kufungwa kutokana na deni la pango.
