HABARI za kusikitrisha ni kwamba, watu sita akiwemo mama wa familia, watoto wake watatu wa kiume na majirani zake waiwili wamefariki dunia baada ya kudaiwa kula ugali ulioandaliwa kwa kutumia unga wa muhogo juzi Jumanne eneo la Ogaminana lililopo Okene, katika Mji wa Kogi nchini Nigeria.
Taarifa zimeeleza kuwa vifo vitatu kutokana na tukio hilo vilitokea Jumatatu ambapo wengine watatu walifariki siku iliyofata wakati wakitibiwa katika Hospitali ya Okene.
Ofisa wa Serikali, kwenye eneo hilo, Bw. Abdulhamid Salahudeen, amesema kuwa mama huyo alinunua unga wa muhogo Jumapili kutoka kwa muuzaji ambaye wanaishi naye kijiji cha jilani cha Ohuepe.
Baadaye mama huyo aliandaa chakula cha usiku huku akipika ugali kwa kutumia unga huo, ambapo pia aliwagawia majilani zake hao sehemu ya ugali huo ili wapate chakula cha usiku.
Baada ya kula mama huyo na watoto wake wawili ndiyo walitangulia kuaga dunia baada ya kupatwa na maumivu makali ya tumbo usiku ule yaliyopelekea kuondoa uhai wao.
Majilani ndiyo walikuwa wa kwanza kugundua kuwa huenda ugali ule ndiyo umesababisha vifo vya watu hao jambo ambalo lilipelekea na wao kwenda Hospitali ya Okene haraka usiku ule pamoja na mtoto mmoja wa marehemu, ambapo licha ya kutibiwa watu hao watatu walifariki dunia Jumanne mchana.