×

Kanye West Afuta Post Zote Instagram

 

Rapa anayetikisa na albamu yake ya DONDA, Kanye West amefuta post zake  zote katika ukurasa wake wa mtandao wa Instagram kufuatia kifo cha rafiki yake kipenzi Virgil Abloh kilichotokea Novemba 28, 2021.

Abloh amefariki kutokana na ugonjwa wa saratani uliomsumbua kwa muda mrefu, Abloh alikuwa mbunifu wa mavazi  na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya mitindo ya Off-White, hadi sasa Kanye West bado hajazungumza chochote kuhusu kuondokewa na rafiki yake kipenzi.

Cc; @bakarimahu

Leave a Comment