Rais Samia Atoa Pole kwa Familia ya Mbunge Halima Nassor, Maziko Kufanyika Leo Kigamboni

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za rambirambi kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Azzan Zungu, kufuatia kifo cha Halima Idd Nassor, Mbunge wa Viti Maalum wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kupitia kundi la wafanyakazi, kilichotokea leo, Januari 18, 2026.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisi ya Bunge, mazishi ya Marehemu Halima Idd Nassor yatafanyika leo Jumapili, Januari 18, 2026, saa 10 jioni katika Makaburi ya Kibada kwa Dole, Kigamboni, jijini Dar es Salaam.
Halima alifariki dunia leo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, jijini Dar es Salaam, alipokuwa akipatiwa matibabu. Msiba upo nyumbani kwake Kigamboni, jijini Dar es Salaam.


