×

Lissu Afikishwa Mahakama Kuu Kesi ya Haki ya Faragha Gerezani – Picha

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, amefikishwa tena katika Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam leo, Julai 23, 2026, kuendelea na shauri linalohusu madai ya ukiukwaji wa haki ya faragha dhidi ya Mamlaka ya Gereza la Ukonga.

Lissu amefikishwa mahakamani hapo akiwa na timu yake ya mawakili, ambao wanaendelea na mchakato wa kisheria kupinga kile wanachodai kuwa ni kuingiliwa kwa haki ya faragha wakati akiwa gerezani.

Shauri hilo linahusisha maombi yaliyowasilishwa na mawakili wake dhidi ya Mamlaka ya Gereza la Ukonga, wakitaka mahakama itoe uamuzi kuhusu masuala yanayohusu haki za msingi za mteja wao.

Kesi hiyo inaendelea kufuatiliwa huku ikitarajiwa kutoa mwelekeo kuhusu namna haki za faragha za wafungwa na mahabusu zinavyopaswa kulindwa kwa mujibu wa sheria.

 

Leave a Comment