×

Mashahidi Wanane Kutoa Ushahidi Katika Kesi ya Mkwepu

Mfanyabiashara na aliyekuwa Mwenyekiti wa Eneo la Goba, Shafii Mkwepu, amekana mashtaka yanayomkabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, baada ya kusomewa hoja za awali mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Beda Nyaki.

Upande wa mashtaka ulidai kuwa Desemba 20, 2017, mlalamikaji Respicious Shayo alinunua kiwanja kutoka kwa Mkwepu kwa Sh milioni 60 na baadaye akalipa Sh milioni 2 za ziada kwa gharama za upimaji. Fedha hizo zilidaiwa kuingizwa katika akaunti ya Mkwepu ya CRDB.

Ilidaiwa kuwa mwaka 2022, Shayo alipofika kwenye kiwanja alikuta tayari kimeuzwa kwa mtu mwingine, jambo lililomsukuma kutoa taarifa polisi na kusababisha Mkwepu kufikishwa mahakamani.

Baada ya kusomewa hoja hizo, Mkwepu alikana mashtaka yote isipokuwa majina na anuani yake. Upande wa Jamhuri ulisema utawasilisha mashahidi wanane na vielelezo vitatu, huku kesi ikiahirishwa hadi Agosti 17, 2026, kwa ajili ya kuanza kusikilizwa. Mshtakiwa amerudishwa rumande.

Leave a Comment