×

Darassa, Roma Kufunikana Nichane Nikuchane, Dar Live

darasa Darassa

Hebu vuta picha usiku mmoja unakwenda kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Burudani wa DAR LIVE halafu unakuta wasanii wa kibabe kama Darassa na ROMA wapo juu ya jukwaani kwa ajili ya kukurusha.

Nini kitatokea?

Unahisi nani atamfunika mwenzake?

Unahisi Darassa anaweza kumfunika ROMA au ROMA anaweza kumfunika Darassa?

romaRoma

Kama ulikuwa unatamani kuona kitu kama hicho, ondoa shaka, ni katika Mkesha wa Mwaka Mpya ndani ya uwanja huohuo wa burudani uliopo Zakhem, Mbagala, washikaji wawili watapiga mpambano wa kufa mtu, mpambano wa kibabe wa NICHANE NIKUCHANE ambao utaamuliwa na wewe mwenyewe kwamba nani kamfunika mwenzake.

Unataka kuliona? Hautaki kuhadithiwa, si ndiyo? Basi utaweza kuliona shindano hili kwa gharama kiduchu tu, yaani kama kumsukuma mlevi kwenye mteremko wa mlima, utatoa mchongo wa buku tano tu mlangoni halafu unazama ndani ambapo huko kuna vinjwaji vya kila aina ambavyo utavipata kwa bei sawa na bure, utafuatilia tangu mwanzo mpaka mwisho, yaani kwa kifupi usiku wa siku hiyo utakuwa ni kuweka mikono juu mwendo wa mateka.

ILIKUPITA HII?

Mpaka Home; Haya Ndo’ Maisha Halisi ya Darassa, Cheki Video Akipika Msosi Gheto