
WATU mbalimbali wanazidi kujitokeza kujaza kuponi kwa ajili ya Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba ambayo inaendelea kwa sasa chini ya Kampuni la Global Publishers wachapishaji wa magazeti ya Uwazi, Championi, Ijumaa, Amani na Risasi.
Ambapo leo, Mr Shinda Nyumba kwa mara nyingine anazidi kuipasua mitaa ya Dar na leo akiwa pamoja na timu ya Shida Nyumba mitaa ya Tegeta na Kunduchi amezidi kusepa na kijiji kufuatia watu wengi kuendelea kujitokeza kujaza kuponi huku wakimshangaa kutokana na urefu wake.








Mbali na kugawa vipeperushi na kusaidia wasomaji wa magazeti ya Global kujaza kuponi, Mr. Shinda Nyumba aliweza kutoa zawadi za sabuni kwa wakazi wawili wa Tegeta Samo Hossea na Ally Ramadhani baada ya kuchezesha droo ya zawadi za papo kwa hapo.
Kwa stori zote kali, Tu-follow
Facebook @Globalpublishers
Twitter @GlobalHabari
Instagram @GlobalPublishers
YouTube @GlobalTVTZ