10 Waripotiwa Kufariki Kwenye Mlipuko wa Bomu Ndani ya Hoteli, Mogadishu

WATU 10 wameripotiwa kufariki kufuatia mlipuko uliotokea kwenye Hoteli moja mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.
Serikali pamoja na vyombo vya Habari nchini humo vimeripoti kuwa shambulio hilo limetekelezwa na kundi la kigaidi la Al-Shabab ambao wanadaiwa kuivamia Hoteli ya Hayat inayosadikika kuwa inatembelewa mara kwa mara na viongozi wa serikali.

Hussein Mohamed mwandishi wa Habari wa kujitegemea aliripoti kwa shirika la utangazaji la Al Jazeera kuwa zilisikika sauti za risasi pia kutoka ndani ya Hoteli ambayo yalikuwa ni majibizano kati ya walinzi wa viongozi wa serikali pamoja na magaidi wa Al Shabab.
“Tayari Al Shabab wameshathibitisha kuhusika katika tukio hilo kwani wametoa taarifa inayobainisha kuwa wamewashikilia baadhi ya viongozi wa serikali na wanasiasa ingawa hwajawataja majina, ingawa kikundi hicho kimekuwa na desturi ya kutekeleza mashambuliji Jijini Mogadishu pamoja na maeneo mengine ya nchi.” alisema Mohamed