×

Droo ya Kwanza ya Shinda Nyumba… Leo Ndiyo Leo, Mbagala Zakhem

DAR ES SALAAm: DROO ya kwanza ya bahati nasibu ya Shinda Nyumba awamu ya pili itachezwa leo katika Viwanja vya Mbagala Zakhem, jijini Dar ambapo washindi watajipatia zawadi za pikipiki, televisheni, simu za kisasa na vyombo vya nyumbani.

Mr. Shinda Nyumba akimuelekeza msomaji namna ya kushiriki Shinda Nyumba.

Kwa mujibu wa Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho, droo hiyo ndogo ni ishara ya kuanza rasmi kwa droo nyingi ndogondogo zitakazofanyika pia hadi mikoani, kuelekea droo kubwa ambayo itamtoa mshindi wa nyumba ya mamilioni ya shilingi iliyojengwa Dar.

Aliwataka wasomaji wa magazeti ya Global Publishers, ambayo ni Risasi, Championi, Uwazi, Amani, Ijumaa na Ijumaa Wikienda kuendelea kusoma na kujaza kuponi ili wajiweke katika nafasi nzuri ya kuibuka mshindi.

Mr. Shinda Nyumba akipiga picha ya pamoja na wasomaji

“Kuponi zote zitakazopokelewa zitashiriki katika droo zote, hata zile zitakazochezwa mikoani, kwa hiyo mtu anakuwa katika nafasi nzuri ya kupata ushindi endapo atakuwa na kuponi nyingi, ingawa siku zote bahati ni bahati, mshindi anaweza kushinda hata kwa kujaza kuponi moja tu,” alisema Mrisho.

PICHA: Richard Bukos | GLOBAL PUBLISHERS

Kwa stori zote kali, Tu-follow

Facebook @Globalpublishers

Twitter @GlobalHabari

Instagram @GlobalPublishers

YouTube @GlobalTVTZ

Shinda Nyumba Awamu ya Pili Yatikisa Jiji la Dar es Salaam