×

Marry You ya Diamond, Ne-Yo Yaibua Ishu

Daimond Platnumz (kushoto) na Ne-yo

Na MWANDISHI WETU| GAZETI LA IJUMAA| MAKALA

ILE ngoma ya Marry You iliyoimbwa na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ akimshirikisha staa wa Muziki wa R&B kutoka Marekani, Shaffer Smith ‘Ne-Yo’ imeibua ishu mtandaoni baada ya Diamond kuwaambia mashabiki wake kuwa imeingia kwenye 10 Bora za ngoma kali zinazoandaliwa na Official Chart Company nchini Uingereza jambo ambalo ilibainika si kweli.

Diamond Platnumz

Siku chache baada ya kutoka ngoma hiyo, Diamond aliingia katika kurasa zake za mitandao ya kijamii na kushukuru media za Uingereza kuiwezesha ngoma hiyo kufanya vizuri.

“Wiki hii tumekusogezea tena 10 bora za Uk ambayo ina ngoma kali za wiki,” aliandika Diamond.

 

Baada ya kuachia maneno hayo sambamba na picha, baadhi ya mashabiki waliingia katika mtandao wa burudani wa UK na kuibuka na chati za 10 bora ambapo ngoma hiyo haikuwepo katika listi.

Hata hivyo, mmoja wa watu wa karibu na Diamond ambaye hakupenda kuchorwa jina lake gazetini, alifafanua ishu hiyo kuwa, Diamond alimaanisha kuwa ngoma hiyo itakuwepo kama bonus track wiki hii.