Makamu Nchimbi Kwenye Mazishi ya Munde Tambwe Tabora

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Emmanuel Nchimbi, amewasili katika Kata ya Cheyo, Manispaa ya Tabora mkoani Tabora, kushiriki msiba wa marehemu Munde na kutoa pole kwa familia, ndugu, jamaa pamoja na wananchi wa eneo hilo.

Katika msiba huo, viongozi mbalimbali wa kitaifa na wa Serikali wameungana na waombolezaji, akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Tabora, Upendo Wella, pamoja na aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, ambao walitoa salamu za rambirambi kwa familia ya marehemu.


