The House of Social Media
gunners X

Waziri Mkuu Afanya  Mazungumzo  Na Waziri Wa Mambo  Ya  Nje Fedha  Na Taasisi  Ya  Kuke Ya Poland

0

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba amefanya mazungumzo na viongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Wizara ya Fedha pamoja na Taasisi ya Usafirishaji wa Bima ya Mikopo (KUKE) kutoka nchini Poland ofisini kwa Waziri Mkuu,  Bungeni jijini Dodoma leo Februari 4, 2026.

Viongozi hao wamejadili kuhusu utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimkakati ikiwemo Mradi wa Reli ya Kisasa (SGR kipande cha 3 na 4) pamoja na kujadili fursa za kuimarisha ushirikiano wa kifedha baina ya Tanzania na Serikali ya Poland.
Leave A Reply