The House of Favourite Newspapers
gunners X

Mfanyabiashara Keko Ashinda Mil. 10 za Magift Pesa

0

Dar es Salaam, Tanzania – Kampeni ya “Magift ya Mixx Pesa,” inayoendeshwa na Kampuni ya huduma za kifedha kwa njia ya simu, Mixx imeendelea kuwafikia Watanzania wengi zaidi, na leo imemfanya mfanyabiashara John Kaseka Kabalo, mkazi wa Keko, kuwa mshindi wa kitita cha shilingi milioni 10.

Kampeni hii ilizinduliwa tarehe 02 Desemba 2025 kama sehemu ya msimu maalum wa sikukuu mwishoni mwa mwaka kwa kuwazawadia watanzania na imeendelea kuleta msisimko mkubwa kwa watumiaji wa huduma za Mixx nchini.

Hadi sasa, kampeni imeshawafikia na kunufaisha zaidi ya Watanzania 40, huku washindi kukiwa na washindi wa kila siku, na wiki ili kuhakikisha wateja wengi zaidi wanapata nafasi ya kushinda.

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi hiyo, Mkurugenzi wa Yas Kanda ya Dar es Salaam Kusini, Bw. Robert Kasulwa, alisema kuwa mafanikio hayo ni kielelezo cha dhamira ya Mixx katika kuwawezesha Watanzania kupitia huduma bora na rafiki za kifedha.

“Tangu kampeni ianze mwezi Desemba, tayari tumeshatoa zaidi ya shilingi milioni 50 kwa washindi 40 kutoka maeneo mbalimbali nchini. Mixx inaamini katika kuleta mabadiliko chanya kwenye maisha ya watumiaji wake kupitia huduma rahisi, salama na za uhakika,” amesema Kasulwa.

Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kifedha na Malipo Kidijitali kutoka Mixx, Ndugu Mshama Mshama alisema kuwa kampeni hiyo ni sehemu ya mkakati mpana wa kuongeza ujumuishi wa kifedha nchini kupitia miamala ya simu.

“Kuwawezesha wananchi ni kutambua mchango wao na kuendeleza juhudi za kuhakikisha kila Mtanzania anapata fursa ya kutumia huduma za kifedha kidijitali kwa urahisi na usalama,” alisema.

Naye mshindi wa milioni 10, John Kaseka, ameishukuru Kampuni ya Mixx na kusema kuwa ushindi wake utamsaidia kufanya mabadiliko makubwa kwenye maisha yake.

“Fedha hizi zitanisaidia kupanua biashara yangu na kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo ada za shule za watoto wangu. Nawashauri Watanzania wenzangu kutumia Mixx kwani fursa zipo na zinaonekana,” alisema kwa furaha.

Kampeni ya Magift ya Mixx Pesa inaendelea kote nchini, na wateja wote wa Mixx wanahimizwa kushiriki kwa kufanya miamala mbalimbali kupitia huduma za Mixx ili kujiongezea nafasi ya kuwa washindi wa zawadi za kila siku, kila wiki na zawadi kubwa za mwisho wa kampeni ambayo ni shilingi milioni 50.

Leave A Reply