Barbara Apigwa Faini ya Laki Tano

KAMATI ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi Kuu Tanzania Bara TBLP katika kikao chake cha Desemba 30, 2021 ilipitia mwenendo wa matukio mbalimbali na kufanya maamuzi yafuatayo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba Barbara Gonzalez ametozwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa kosa la kuishutumu Bodi ya ligi kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii kuwa ilimzuia yeye na familia yake kuingia uwanjani kutazama mchezo kati ya Simba dhidi ya Yanga.
Barbara hakubaliana na maelekezo halali ya maafisa wa mchezo huo kuhusu utaratibu wa kuingia eneo maalum VVIP ndipo akamua kuondoka.


