Tarura Yatoa Ufafanuzi Kuhusu Faini Zinazotokana na Kukwepa Ushuru wa Maegesho

WAKALA wa barabara Mijini na Vijijini Tarura umetoa taarifa kwa umma kuwa umeanza rasmi kutoza faini kwa watumiaji wa maegesho waliopitisha siku 14 bila kulipa madeni ya ushuru wa maegesho.
Kwa mujibu wa kanuni ya 9 (3) ya kanuni za Serikali za Mitaa (Mamlaka ya Miji) ( Usimamizi na Uendeshaji wa Maegesho ya Vyombo vya Usafiri katika Hifadhi za Barabara) Tangazo la Serikali namba 799 lililochapishwa Desemba 3 2021.
“Kila mmiliki wa chombo cha usafiri kinachoegeshwa katika maegesho atakuwa na wajibu wa kulipa ushuru wa maegesho kwa namna na viwango vilivyoainishwa katika kanuni, endapo mmiliki wa chombo atashindwa kulipa ushuru wa maegesho baada ya siku 14 tangu alipoondoa chombo cha usafiri katika maegesho, mmiliki huyo atakuwa amekaidi na atawajibika kulipa faini ya shilingi 10000/=
Tarura wameendelea kusisitiza kuwa mtumiaji wa huduma ya maegesho anatakiwa kupiga namba *152*00# ili kupata huduma zote ikiwemo kujua kiasi cha deni lakini pia kulipa ushuru.