The House of Favourite Newspapers
gunners X

Ukiokota Chaja ya Simu ya Aina Hii Umekwisha! Ukichomeka Kwenye Simu, Unadukuliwa

0

Wahenga chali, cha kuokota siyo cha kuiba tena! Unaokota halafu unaibiwa! Vuta picha upo kwenye mishe zako mara unaona ‘charger’ ya simu, tena mpya kabisa!

Bila shaka utaiokota na kuificha haraka ukiamini umeokota dodo chini ya mpera!

Harakaharaka utaenda kuijaribu kama ni nzima kwa kuichomeka kwenye simu yako au kompyuta yako na kuunganisha na simu! Sikia hii, ukifanya hivyo tu, umekwisha!

Utadukuliwa na hautaamini macho yako kama wahenga! Kivipi?

Wadukuzi (hackers) wamekuja na ‘mbwinu’ mpya. Wamegundua kifaa kiitwacho O.MG Elite Cable ambacho kinafanana kila kitu na chaja za kawaida za simu, iwe ni android au Iphone, iwe ni Type C au chaja za kawaida!

Kinachofanyika ni kwamba, tofauti na chaja za kawaida, O.MG Elite Cable inakuwa na ‘network access point’ ndogo isiyoonekana kwa macho.

Wanachokifanya wadukuzi, ni kuitupa cable hii mahali wanapopalenga kudukua, iwe ni ofisini kwako, nyumbani au sehemu yoyote, kisha wanakaa mitaa hiyohiyo kusubiri mchongo utiki.

Ukiichomeka tu kwenye simu yako, itaonesha inaingiza chaji lakini kumbe kinachofanyika ni kitu tofauti kabisa!

Ile network access point itatuma signal kwa mfumo wa Wifi kwenda kwenye kifaa cha mdukuzi ambapo harakaharaka atajiunga kama unavyoconnect wifi na mpaka hapo, tayari atakuwa na uwezo wa kuona na kufanya chochote kwenye simu yako bila mwenyewe kugundua.

Miongoni mwa mambo anayoweza kuyafanya, ni pamoja na kuziona password zote zilizopo kwenye simu yako, taarifa za kifedha, picha na taarifa zote za siri zilizopo kwenye simu yako.

Si hivyo tu, atakuwa na uwezo wa kudownload application za udukuzi na kuzi-install kwenye simu yako bila wewe kuwa na taarifa.

Kwa kifupi utakuwa umedukuliwa! Na hapo sasa atakuwa na uwezo wa kufanya chochote anachokitaka, ikiwemo kuhamisha fedha, kujitumia picha na taarifa zako zote muhimu!

Inshort utakuwa umekwisha! Ukiipata hii, msanue na mwenzako, usiokote charger na kuichomeka kwenye simu yako, hata kama inavutia kiasi gani!

Ukitaka charger, kanunue mpya kwa wauzaji wanaoaminika! Mgunduzi wa O.MG Elite Cable, Mike Grover anasema kifaa hiki kinaweza kusoma signal mpaka umbali wa mita 90!

Usikae kizembe mjini, watu wapo kazini!

Leave A Reply